وَلَمَّا سُقِطَ فِيٓ أَيۡدِيهِمۡ وَرَأَوۡاْ أَنَّهُمۡ قَدۡ ضَلُّواْ قَالُواْ لَئِن لَّمۡ يَرۡحَمۡنَا رَبُّنَا وَيَغۡفِرۡ لَنَا لَنَكُونَنَّ مِنَ ٱلۡخَٰسِرِينَ
Na walipo juta na wakaona ya kwamba wamekwisha potea, walisema: Ikiwa Mola wetu Mlezi hakuturehemu na akatusamehe, bila ya shaka tutakuwa miongoni mwa walio khasiri.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Na walipojuta wale walioabudu kigombe badala ya Mwenyezi Mungu pale aliporudi Mūsā kwao, na wakaona kwamba walipotea njia ya sawa, na waliondoka kwenye dini ya Mwenyezi Mungu, walianza kuukubali uja na kuomba kufutiwa makosa yao wakasema, «Mola wetu Asipoturehemu kwa kukubali toba yetu, na kufinika kwayo madhambi yetu, tutakuwa ni wenye kuangamia ambao matendo yao mema yamepita bure.»
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس