قَالَ فِرۡعَوۡنُ ءَامَنتُم بِهِۦ قَبۡلَ أَنۡ ءَاذَنَ لَكُمۡۖ إِنَّ هَٰذَا لَمَكۡرٞ مَّكَرۡتُمُوهُ فِي ٱلۡمَدِينَةِ لِتُخۡرِجُواْ مِنۡهَآ أَهۡلَهَاۖ فَسَوۡفَ تَعۡلَمُونَ
Akasema Firauni: Mmemuamini kabla sijakupeni idhini? Hizi ni njama mlizo panga mjini mpate kuwatoa wenyewe. Lakini karibu mtajua!
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Fir'awn akasema kuwaambia wachawi, «Mumemuamini Mwenyezi Mungu kabla sijawapa idhini mumuamini? Hakika kumuamini kwenu Mwenyezi Mungu, kumsadiki kwenu Mūsā na kuukubali kwenu unabii wake ni hila mlizozipanga nyinyi na Mūsā ili muwatoe watu wa mji wenu kutoka humo, na ili muzivamie heri zake na mufaidike nazo peke yenu.Basi mtajua, enyi wachawi, adhabu na mateso yatakayowashukia nyinyi.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس