وَٱذۡكُر رَّبَّكَ فِي نَفۡسِكَ تَضَرُّعٗا وَخِيفَةٗ وَدُونَ ٱلۡجَهۡرِ مِنَ ٱلۡقَوۡلِ بِٱلۡغُدُوِّ وَٱلۡأٓصَالِ وَلَا تَكُن مِّنَ ٱلۡغَٰفِلِينَ
Na mkumbuke Mola Mlezi wako nafsini kwako kwa unyenyekevu na khofu, na bila ya kupiga kelele kwa kauli, asubuhi na jioni. Wala usiwe miongoni wa walio ghafilika.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Na mtaje Mola wako, ewe Mtume, ndani ya nafsi yako kwa kumnyenyekea Mwenyezi Mungu na kumdhalilikia, hali ya kumcha Yeye moyoni, na umuombe kwa namna ya kati na kati baina ya kutoa sauti na kuifanya chini, katika mwanzo wa mchana na mwisho wake, na usiwe ni miongoni mwa wenye kughafilika kumtaja Mwenyezi Mungu na kupumbaa katika nyakati zao zinginezo.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس