وَإِذۡ تَأَذَّنَ رَبُّكَ لَيَبۡعَثَنَّ عَلَيۡهِمۡ إِلَىٰ يَوۡمِ ٱلۡقِيَٰمَةِ مَن يَسُومُهُمۡ سُوٓءَ ٱلۡعَذَابِۗ إِنَّ رَبَّكَ لَسَرِيعُ ٱلۡعِقَابِ وَإِنَّهُۥ لَغَفُورٞ رَّحِيمٞ
Na pale alipo tangaza Mola wako Mlezi kwamba hapana shaka atawaletea watu ambao watawaadhibu kwa adhabu mbaya mpaka Siku ya Kiyama. Hakika Mola wako Mlezi ni Mwepesi wa kuadhibu, na bila ya shaka ni Mwenye maghfira, na Mwenye kurehemu.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Na kumbuka, ewe Mtume, pindi Alipotangaza Mola wako, tangazo wazi, kwamba Atawapelekea Mayahudi mwenye kuwaonjesha adhabu mbaya na kuwadhalilisha mpaka Siku ya Kiyama. Hakika Mola wako ni Mpesi wa kutesa kwa anayestahili kuteswa kwa sababu ya ukafiri wake na uasi wake. Na hakika Yeye ni Mwingi wa kusamehe dhambi za wenye kutubia, ni Mwnye huruma kwao.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس