سَيَقُولُ ٱلَّذِينَ أَشۡرَكُواْ لَوۡ شَآءَ ٱللَّهُ مَآ أَشۡرَكۡنَا وَلَآ ءَابَآؤُنَا وَلَا حَرَّمۡنَا مِن شَيۡءٖۚ كَذَٰلِكَ كَذَّبَ ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِمۡ حَتَّىٰ ذَاقُواْ بَأۡسَنَاۗ قُلۡ هَلۡ عِندَكُم مِّنۡ عِلۡمٖ فَتُخۡرِجُوهُ لَنَآۖ إِن تَتَّبِعُونَ إِلَّا ٱلظَّنَّ وَإِنۡ أَنتُمۡ إِلَّا تَخۡرُصُونَ
Watasema walio shirikisha: Lau kuwa Mwenyezi Mungu ange taka tusingeli shiriki sisi, wala baba zetu; wala tusingeli harimisha kitu chochote. Vivi hivi walikanusha walio kuwa kabla yao mpaka walipo onja adhabu yetu. Sema: Je, nyinyi mnayo ilimu mtutolee? Nyinyi hamfuati ila dhana. Wala hamsemi ila uwongo tu.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Watasema wale walioshirikisha, «Lau Mwenyezi Mungu Alitaka tusishirikishe, sisi na baba zetu, na tusihararamishe kitu chochote kinyume na matakwa Yake, hatungalifanya hilo.» Hapo Mwenyezi Mungu Aliwarudi kwa kuwaeleza kwamba utata huu ulivumishwa na makafiri kabla yao, wakautumia kuukanusha ulinganizi wa Mitume wao na wakaendelea kufanya hivyo mpaka ikawateremkia adhabu ya Mwenyezi Mungu. Waambie, ewe Mtume, «Je, mnayo elimu sahihi mtuoneshe, juu ya wanyama howa na makulima mliyoharamisha na juu ya madai yenu kwamba Mwenyezi Mungu Aliwatakia ukafiri, Akauridhia kwenu na Akaupendelea kwenu? Hamuna mnachofuata, katika mambo ya dini, isipokuwa dhana tu; na hamukuwa nyinyi isipokuwa mnasema urongo.»
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس