وَعَلَى ٱلَّذِينَ هَادُواْ حَرَّمۡنَا كُلَّ ذِي ظُفُرٖۖ وَمِنَ ٱلۡبَقَرِ وَٱلۡغَنَمِ حَرَّمۡنَا عَلَيۡهِمۡ شُحُومَهُمَآ إِلَّا مَا حَمَلَتۡ ظُهُورُهُمَآ أَوِ ٱلۡحَوَايَآ أَوۡ مَا ٱخۡتَلَطَ بِعَظۡمٖۚ ذَٰلِكَ جَزَيۡنَٰهُم بِبَغۡيِهِمۡۖ وَإِنَّا لَصَٰدِقُونَ
Na wale walio fuata dini ya Kiyahudi tumewaharimishia kila mwenye kucha. Na katika ng'ombe na kondoo na mbuzi tumewaharimishia shahamu yao, isipo kuwa ile iliyo beba migongo yao au matumbo yao, au iliyo gandamana na mifupa. Tuliwalipa hivyo kwa sababu ya uasi wao. Na bila ya shaka Sisi ndio wasema kweli.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Na watajie washirikina hawa, ewe Mtume, wanyama na ndege tuliowaharamishia Mayahudi: nao ni kila ambaye hana pasuko vidoleni mwake, kama ngamia na mbuni, na mafuta ya ng’ombe, mbuzi na kondoo isipokuwa yale mafuta yaliyoshikana na migongo ya wanyama hao na tumbo zao, au yaliyoshikana na mfupa wa mkia na mbavu na mfano wake. Uharamishaji huu uliotajwa juu ya Mayahudi ni adhabu kutoka kwetu kwa sababu ya matendo yao maovu. Na sisi ni wakweli kwa yale tuliyoyaeleza kuhusu wao.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس