وَيَقُولُ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ أَهَـٰٓؤُلَآءِ ٱلَّذِينَ أَقۡسَمُواْ بِٱللَّهِ جَهۡدَ أَيۡمَٰنِهِمۡ إِنَّهُمۡ لَمَعَكُمۡۚ حَبِطَتۡ أَعۡمَٰلُهُمۡ فَأَصۡبَحُواْ خَٰسِرِينَ
Na walio amini watasema: Hivyo hawa ndio wale walio apa ukomo wa viapo vyao kuwa wao wa pamoja nanyi? Vitendo vyao vitapotea bure, na wataamkia kuwa wenye kukhasirika.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Wakati huo watasema baadhi ya Waumini kuwaambia wengine, wakionea ajabu hali ya wanafiki, pindi mambo yao yatakapofichuka, «Je, hawa ndio wale ambao waliapa viapo vizito kwamba wao wako nasi?» Zimebatilika amali za wanafiki walizozifanya ulimwenguni, hawana malipo mema ya amali hizo, kwa kuwa wao walizifanya bila ya Imani. Hapo basi, wamepata hasara ya ulimwenguni na Akhera.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس