هَـٰٓأَنتُمۡ هَـٰٓؤُلَآءِ تُدۡعَوۡنَ لِتُنفِقُواْ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ فَمِنكُم مَّن يَبۡخَلُۖ وَمَن يَبۡخَلۡ فَإِنَّمَا يَبۡخَلُ عَن نَّفۡسِهِۦۚ وَٱللَّهُ ٱلۡغَنِيُّ وَأَنتُمُ ٱلۡفُقَرَآءُۚ وَإِن تَتَوَلَّوۡاْ يَسۡتَبۡدِلۡ قَوۡمًا غَيۡرَكُمۡ ثُمَّ لَا يَكُونُوٓاْ أَمۡثَٰلَكُم
Angalieni! Nyinyi mnaitwa mtumie katika njia ya Mwenyezi Mungu, na wapo katika nyinyi wanao fanya ubakhili. Na anaye fanya ubakhili basi anajifanyia ubakhili mwenyewe. Na Mwenyezi Mungu si mhitaji, na nyinyi ndio wahitaji. Na mkigeuka atawaleta watu wengine badala yenu, nao hawatakuwa kama nyinyi.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Haya nyini, enyi Waumini, mnaitwa kutoa kwenye kupigana jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu na kuinusuru Dini Yake. Basi miongoni mwenu kuna anayefanya uchoyo kutoa katika njia ya Mwenyezi Mungu. Na mwenye kufanya uchoyo huwa anajifanyia uchoyo nafsi yake. Na Mwenyezi Munmgu, Aliyetukuka, Ndiye Mkwasi wa kutowahitajia nyinyi, na nyinyi ndio mnaomhitajia Yeye. Na mkipa mgongo mkaacha kumuamini Mwenyezi Mungu na kufuata amri Zake, Atawaangamiza na Atawaleta watu wengine, na kisha wasiwe ni kama nyinyi katika kuzipa mgongo amri za Mwenyzi Mungu, bali wao watamtii Yeye na kumtii Mtume Wake na watapigana jihadi katika njia Yake kwa mali yao na nafsi zao.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس