وَلَا يَتَمَنَّوۡنَهُۥٓ أَبَدَۢا بِمَا قَدَّمَتۡ أَيۡدِيهِمۡۚ وَٱللَّهُ عَلِيمُۢ بِٱلظَّـٰلِمِينَ
Wala hawatayatamani kabisa, kwa sababu ya iliyo kwisha yatanguliza mikono yao. Na Mwenyezi Mungu anawajua walio dhulumu.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Na wala hawa Mayahudi hawatatamani kifo kabisa kwa vile wanavyoyapenda maisha ya duniani kuliko Akhera na kwa kuogopa kuteswa na Mwenyezi Mungu kwa sababu ya yale waliyoyatanguliza ya ukafiri na matendo maovu. Na Mwenyezi Mungu Anawajua mno madhalimu, hakifichamani Kwake chochote cha udhalimu wao.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس