Al-Juma'ah
يُسَبِّحُ لِلَّهِ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِ ٱلۡمَلِكِ ٱلۡقُدُّوسِ ٱلۡعَزِيزِ ٱلۡحَكِيمِ
Viliomo mbinguni na viliomo katika ardhi vinamtakasa Mwenyezi Mungu, Mfalme, Mtakatifu, Mwenye nguvu, Mwenye hikima.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Vinamtakasa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka vyote vilivyo mbinguni na vyote vilivyo Ardhini, na Yeye Peke Yake Ndiye mfalme wa kila kitu, Aliye Mshindi kwenye utawala Wake bila ya mpinzani, Mwingi wa hekima katika kuyapelekesha mambo Yake na utengenezaji Wake.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس